Kabla ya
mchezo wa jana alhamisi wa kundi D wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ijayo
ya Ulaya (Euro 2016) kati ya England na San Marino swali kubwa ukiachana na
pointi tatu(3) muhimul ilikuwa ni magoli mangapi vijana wa Roy Hodgson
wangeifunga San Marino ambayo kwa takwimu na rekodi mbali mbalimbali pengine
ndiyo timu dhaifu zaidi katika uso wa dunia.
Historia ya
timu hii inayoundwa na wauza mitumba,wafanyakazi wa viwandani na wamiliki wa
baa inaanzia mwaka 1990 ambapo ilishuka dimbani kwa mara ya kwanza kucheza kama
timu kamili ya taifa katika mchezo unaotambuliwa rasmi na mashirikisho ya
soka,tangu hapo wamekuwa wakiweka rekodi za kuzivunja wenyewe.
YAFUATAYO NI
MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU SAN MARINO
1. San Marino wameshinda mchezo mmoja
(1) tu katika historia tena kwa kuwafunga vibonde wengine Liechtenstein 1-0
katika mchezo wa kirafiki hii ikiwa ni mwaka 2004.
2. Katika orodha ya viwango vya ubora
vya FIFA,San Marino wanaburuza mkia wakifungana na taifa la Bhutan katika
nafasi ya 208.
3. Katika michezo mitano waliyokutana na
England wamebamizwa jumla ya magoli 31 huku wao wakifanikiwa kufunga goli 1
tu.(San Marino walifungwa magoli 13 na England katika michezo miwili tu
ya
kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia nchini Brazil)
4. Ndugu wawili mapacha Aldo na Davide
Simoncini waliweka rekodi ya kujifunga katika mchezo ulioisha kwa San Marino
kubugizwa magoli 6-0 na Sweden hii ikiwa ni mwaka 2010.
5. Taifa la San Marino lina wakazi
wapatao 32,000 tu,ambao ni sawa na nusu ya idadi ya watazamaji walijitokea katika mchezo
wa jana pale Wembley.
6. Ligi ya San Marino inaitwa Campionato
Sammarinese di Calcio ambayo wao huifananisha na ligi kuu ya England,katika
vilabu vyote hivyo hakuna hata kimoja chenye uwanja wake hivyo basi kimoja kati
ya viwanja vitano huchagulia kiholela kwa ajili ya ligi kuchezwa.
Uwanja wa taifa wa San Marino unaochukua watu 6,664 |
7. Katika michezo rasmi ambayo San
Marino wamecheza wamefanikiwa kufunga jumla ya magoli 20 tu huku wao
wakibugizwa magoli 536.
8. San Marino bado inahaha kuboresha
kiwango chake katika miaka ya karibuni toka mwaka 2008 mpaka sasa katika
michezo 30 ya kusaka tiketi za kombe la dunia na euro wamefanikiwa kufunga magoli 2 tu na kufungwa
159.
9. Waliweka rekodi mbaya zaidi mwaka
2006 katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya Ulaya (Euro) baada ya
kukubali kichapo cha magoli 13-0 dhidi ya Ujerumani.
10. Goli la Davide Gaulteris la sekunde
ya 7 dhidi ya England mwaka 1993 ndilo linabaki kuwa ni goli la mapema zaidi
katika michezo ya kufuzu kuelekea kombe la dunia,katika mchezo huo San Marino
walifungwa magoli 7-1.
MATOKEO YA JANA
England 5 – 0 San Marino (Wayne Rooney 1,Phil Jagielka 1,Danny Welbeck 1,Della Valle
na Andros Townsend 1)
Uwanja: Wembley 55,990
0 comments:
Post a Comment