Mlinda
mlango aliyepoteza namba katika kikosi cha kwanza cha klabu ya Chelsea Peter
Cech hatimaye amevunja ukimya na kusema kuwa atatimka klabuni hapo ikiwa
ataendelea kusota benchi.
Cech (32) ambaye amepoteza namba tangu kuwasili kwa
mlinda mlango Thibaut Courtois ameshaichezea klabu hiyo jumla ya michezo
472 na
kutwaa mataji kadhaa lakini msimu huu amefanikiwa kucheza jumla ya michezo
miwili tu.
Cech amesema
“Bado sijaongea na yoyote,lakini
nafikiri wananifahamu vizuri kiasi cha kugundua kuwa hali ni tofauti na
nilivyofikiri”
“Euro 2016 inakuja na nikifikiria
hatima yangu timu ya taifa nadhani sina sababu ya kuendelea kukaa benchi”
“Kama hali hii haitapata
jibu,nitatafuta mwenyewe njia ya kutatua “
0 comments:
Post a Comment