Kocha mkuu wa klabu ya Swansea City Garry Monk amesifia
uteuzi wa kiungo wake aliye katika kiwango kizuri Jonjo Shelvey katika kikosi
cha timu ya taifa ya England kilichotajwa leo hii na kocha Roy Hodgson kwa
ajili ya michezo miwili ya kusaka tiketi ya kufuzu kucheza michuano ijayo ya
Ulaya,Euro 2016 dhidi ya San Marino na Estonia.
Monk amesema kuitwa kwa nyota huyo kwa mara nyingine tena
katika kikosi hicho baada ya kufanya hivyo mwaka 2012 kutafungua zaidi milango kwa nyota wakekutambulika
kimataifa.Monk amesema
“Ni habari nzuri kwa Shelvey na klabu kwa ujumla.Tuna wachezaji wengi
wa kimataifa hapa lakini kwa upande wa England tumekuwa hatuna bahati hiyo. Hivyo
kwa uteuzi huo nadhani hii ni nafasi nzuri hata kwa wengine pia kuanza
kutazamwa”
“Watu wanataka England
icheze mpira wa pasi na kushambulia,hii ni aina ya mpira ambao Swansea tumekuwa
tukiucheza kwa kipindi kirefu sasa.Akiongezeka mwingine katika kikosi cha
Hodgson tutashuhudia mpira mzuri sana”.
Mbali ya Shelvey pia Swansea imetoa wachezaj kadhaa katika
timu mbalimbali za taifa kama vile Ki Sung Yueng (Korea),Gylfi Sigurdsson ( Iceland)na
Wilfred Bony (Ivory Coast)
Kikosi kamili kilichotajwa na Roy Hodgson ni kama ifuatavyo…..
GOALKEEPERS
Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
DEFENDERS
Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Southampton), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), John Stones (Everton)
MIDFIELDERS
Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jonjo Shelvey (Swansea City), Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
FORWARDS
Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Welbeck (Arsenal)
0 comments:
Post a Comment