Wakati kikosi cha Yanga
kikitarajiwa kushuka
uwanjani kesho Jumamosi
kupambana na wapinzani wao
wa jadi, Simba, beki wa
kushoto wa timu hiyo, Oscar
Joshua, amenunua viatu
vipya kwa ajili kukabiliana
na washambuliaji wa Simba,
Emmanuel Okwi na Ramadhan
Singano ‘Messi’.
Joshua, mwenyeji wa Mwanza,
amefikia hatua hiyo
kuhakikisha anawadhibiti
vilivyo wachezaji hao ambao
wanasifika kwa kuwa na kasi
kali pindi wanapokuwa
uwanjani.
Mchezaji wa Yanga ambaye
amesema si ishu kubwa yeye
kutajwa, amesema Joshua
amewapania vilivyo
wachezaji hao ambao
wamekuwa chachu ya mabao ya
Simba, kuhakikisha
hawatengenezi nafasi yoyote
ya kufunga katika mechi
hiyo.
“Unajua hivi sasa kuna hali
kama ya mvuamvua, hivyo
ameamua kutafuta viatu
vipya ambavyo vitamsaidia
kutoteleza kila wakati
pindi atakapokuwa
akikabiliana na wachezaji
hao.
“Okwi na Messi wanajulikana
kwa kuwa na chenga za
maudhi, hivyo kama mchezaji
akiwa na viatu ambavyo meno
yake siyo mazuri, wanaweza
kumuaibisha na hilo ndilo
lililomfanya Oscar afanye
hivyo,” kilisema chanzo
hicho cha habari.
0 comments:
Post a Comment