Baada ya kuibuka taarifa kuwa klabu ya Manchester United imeipiku Arsenal katika kiti cha uongozi wa kumtaka kiungo Sami Khedira,taarifa kutoka gazeti la Express zinasema Arsenal imehamishia majeshi yake kwa kiungo Mbrazil Romulo anayekipiga katika klabu ya Spartak Moscow ya Urusi.
Romulo ambaye anaimudu vyema nafasi ya kiungo cha ulinzi kiasi cha kufananishwa na kiungo wa zamani wa Arsenal Gilberto Silva inasemekana anataka kuhama Urusi na kutafuta changamoto katika ligi nyingine kubwa barani Ulaya.
Katika kuonyesha kuwa klabu ya Arsenal imepania kumnasa nyota huyo tayari imeshajiandaa kutoa £9.5m pamoja na mshambuliaji wake Yaya Sanogo kwa mkopo ifikapo mwezi januari.
0 comments:
Post a Comment