Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger
anafikiria kutumia kiasi cha paundi milioni 60 za Uingereza kwa ajili ya
kukiimarisha kikosi chake mwezi januari mwakani.
Wenger ambaye tayari ametumia zaidi ya paundi milioni 70
wakati wa kipindi cha majira ya joto kusajili nyota kama Alexis Sanchez,Calum
Chambers,Danny Welbeck,Mathieu Debuchy na mlinda mlango David Ospina
anahusishwa kuwawinda nyota kama
Sami Khedira,Julian Draxler na Mbrazil
Anderson Talisca.
Kwa mujibu vya vyombo mbalimbali vya habari vya Hispania
taarifa zinasema tayari Arsenal imeshakubaliana kila kitu na kiungo wa Real
Madrid Sami Khedira (27) ikiwemo
mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki kinachosubiriwa kwa sasa ni makubaliano ya
ada ya uhamisho baina ya vilabu hivyo viwili.
Ada ya usajili wa Khedira huenda ikiwa chini ya paundi
milioni 10 kutokana na nyota huyo kuwa katika kipindi cha mwisho kabisa cha
mkataba wake katika klabu ya Real Madrid.
Pia klabu ya Arsenal imejiunga katika mbio za kumsajili
mshambuliaji raia wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Benfica ya Ureno
Anderson Talisca (20).Talsica amevuta hisia za makocha wengi Ulaya baada ya
kuanza msimu wa ligi ya Ureno kwa style ya aina yake baada ya kuifungia Benfica
magoli 6 katika michezo 7 na kuifanya klabu hiyo iendelee kuongoza huku ikiwa
haijapoteza mchezo hata mmoja
.
Talisca ambaye alijiunga na Benfica mwezi Julai kwa ada ya
paundi milioni 3 akitokea klabu ya Bahia ya nyumbani kwao Brazil inasemekana
katika mkataba wake kuna kipengere kinachomruhusu kuhama kwa ada ya paundi
milioni 18.Mbali ya Arsena vilabu vingine vinavyomtolea macho kinda huyo ni
Liverpool,Chelsea na Manchester United.
Taarifa nyingine zinasema kuwa kocha Arsene Wenger
anafikiria tena kufufua ndoto za kumfukuzia kiungo wa klabu ya Shalke 04 ya
Ujerumani Julien Draxler baada ya kumshindwa kumnasa hapo mwezi januari kwa
kile kinachodaiwa dau kubwa la usajili lililotakiwa na klabu yake la paundi
milioni 37.
0 comments:
Post a Comment