Polisi nchini Africa Kusini wameanzisha msako
mkali dhidi ya mtu aliyempiga risasi na
kumuua kipa na kapteni wa timu ya taifa hilo
Senzo Meyiwa.
Ili kufanikisha na kuufanya uchunguzi wao
uwe rahisi na wa haraka,polisi hao wametoa
zawadi nono ya randi 250,000 sawa na dola
za kimarekani 14,000; hadi $23,000 kwa
yeyote atakayefanikisha taarifa za kukamatwa
kwa mtu huyo,ambaye anaongeza namba ya
matukio ya uhalifu yaliyokithiri nchini humo.
Meyiwa, amekufa akiwa na umri wa miaka 27,
inaarifiwa kuwa alipigwa risasi na kuuawa na
mtu aliyeingia nyumbani kwa mpenzi wake na
kutekeleza mauaji hayo.
Rais wa taifa hilo Jacob Zuma ametuma
salamu za rambi rambi na kutoa ujumbe
kwamba maneno hayatoshi kuonesha
mshtuko wa taifa letu kwa kuuawa kwa
Meyiwa.
Polisi wametoa taarifa kuwa si mtu mmoja
bali walikua wanaume wawili waloingia
nyumbani na mmoja alibaki nje ya nyumba
hiyo huko kwenye kitongoji cha
Vosloorus,jijini kusini mwa Johannesburg,na
walipoingia wakadai Meyiwa .
Rais Jacob Zuma amesema kwamba taifa lake
linaomboleza kifo cha mchezaji nguli na
mchanga na kiongozi wa timu ya taifa
ambaye maisha yake yamepokwa angali
mdogo na katika kilele cha mafanikio yake ,
na maneno pekee hayatoshi kuelezea hasara
waliyopata.
Vituo vya redio na runinga vina pokea ujumbe
wa pole kwa kifo cha Meyiwa .
Tukio hilo la kupigwa risasi kwa Meyiwa
kunaonesha taswira ya matumizi mabaya ya
silaha nchini Africa Kusini, ikiwa ni siku
chache tu kesi ya mwanariadha Osca
Pistorious iliporindima nchini humo na
kutolewa maamuzi ambayo hayajawaridhisha
walio wengi nchini humo.
Taifa hilo linajiuliza maswali lenyewe juu ya
kuongezeka kwa matukio ya uhalifu nchini
humo,na wanaouawa ni watu wenye vipaji vya
kipekee kama miaka saba iliyopita aliuawa
nguli wa muziki wa reggae Lucky Dube .
Jambo kubwa na la msingi kwa sasa dunia
imewageukia wanamgambo wa
kiislamu,wakati kuna uhalifu duniani kote.
Meyiwa alizaliwa mnamo tarehe 24
September ,mwaka 1987
Alikuwa ni kipa wa timu kutoka Johannesburg
ya Orlando Pirates
Alijiunga na timu ya taifa hilo mwaka 2013
Mwaka uliofuata alichaguliwa kuwa kapteni
wa timu ya taifa.
Na kuilete nchi yake vikombe saba vya
ushindi alikuwa na mpenzi ambaye ni
muigizaji Kelly Khumalo ambaye alipata naye
mototo mmoja naye.
Meyiwa anatajwa kuwa kipa bora barani
Africa .
0 comments:
Post a Comment