Nyota wa zamani wa kikosi cha timu ya taifa ya England Paul Scholes
ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka amesema kiungo wa Arsenal Jack Wilshere na winga wa
Liverpool Raheem Sterling wanapaswa kuwemo katika kikosi cha vijana cha nchi hiyo
kitakachoshiriki michuano ijayo ya Ulaya hapo mwakani.
Kikosi hicho cha vijana (U21) ambacho mpaka sasa kimeshinda michezo yake
9 kati ya 10 usiku wa leo kitajitupa uwanjani kuvaana na Croatia lakini Scholes
anaona ili kikosi hicho kifanye vizuri hapo mwakani basi hakina budi
kuwajumuisha kikosini nyota hao ili kuongeza makali na uzoefu.
Scholes amesema “England wanapaswa
kuiga mfano wa Hispania hasa kwa kiungo Juan Mata.Mata alikuwa miongoni wa
wachezaji wa Hispania walioiwezesha nchi hiyo kutwaa kombe la dunia mwaka 2010
pale Africa Kusini na akapelekwa tena kwenye kikosi cha vijana cha nchi hiyo na
kukisaidia kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka uliofuata”
“Kama mpango huo ulifanikiwa kwa Juan
Mata kwanini usitumiwe kwa nyota tulionao?”
Alihoji Scholes na kuongeza
“Kikosi cha vijana kikifuzu
nitamshauri kocha wake Southgate awajumuishe pia Wilshere na Sterling japo wana
nafasi kikosi cha wakubwa”
0 comments:
Post a Comment