728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 01, 2014

    DROGBA AWAPANDISHA WAZIMU GALATASARAY KUIUA ARSENAL



    Mshambuliaji mwenye rekodi nzuri na ya pekee yake ya kuifunga klabu ya Arsenal karibu kila mara achezayo dhidi yake Muivory Coast Didier Drogba jana jumanne alifika katika dimba la Emirates ambapo wachezaji wa iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Galatasaray walikuwa wakifanya maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya mtanange wa leo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Arsenal na kuwatakia ushindi Waturuki hapo katika mchezo wa leo jumatano usiku.



    Drogba ambaye alijiunga na
    Galatasaray kwa uhamisho huru akitokea klabu ya Shanghai Shenhua januari 2013  alifanikiwa kuifungia klabu hiyo magoli 20 (mawili ya karibuni yakiwa dhidi ya Arsenal katika michuano ya Emirates Cup) huku akitengeneza mengine 13.Mpaka sasa Drogba ameifunga magoli 15 yakiwa ni sawa na idadi aliyocheza dhidi ya klabu hiyo ya London kaskazini.


    Hakuishia tu kuhudhuria mazoezi hayo kwani mbali na kutoa jezi yake iliyokuwa imesainiwa pia Grogba aliwapa wenzake hao ambao kwa sasa wako chini ya kocha Cesare Prandeli mbinu kadhaa za kuibamiza Arsenal katika dimba lake la nyumani na hatimaye kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele zaidi katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu na yenye utajiri wa kutupwa.
    Galatasaray wakishangilia ushindi wa kombe la Emirates


    DONDOO MUHIMU KUELEKEA MCHEZO HUO!!

    Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa vilabu hivyo kukutana katika michuano ya Ulaya baada ya hapo awali kukutana katika mchezo wa fainali wa Uefa Cup 2000 (sasa Europa League)ambapo Galatasaray ilishinda kwa penati 4-1.

    Mbali ya penati hizo,Arsenal haijawahi kupoteza mchezo dhidi ya klabu yoyote ya Uturuki ikiwa imeshinda michezo mitano (W5) na kutoka sare mara nne (D4)ikizuia kufungwa bao katika michezo minane kati ya tisa iliyocheza dhidi ya vilabu vya nchi hiyo.


    Galatasarary haijawahi kushinda mchezo wowote wa Ulaya dhidi ya klabu yoyote ya England (D3,L6) huku ikiwa na rekodi ya kuvuna kadi nyekundu moja katika kila michezo sita.

    Galatasaray imezuia kufungwa goli katika mchezo mmoja (1)  tu kati ya kumi na nne (14) iliyopita ya Ulaya
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DROGBA AWAPANDISHA WAZIMU GALATASARAY KUIUA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top