Kiingilio cha chini kwenye mechi ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya
Yanga na Simba itakayochezwa
Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni
sh. 7,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio
hicho ni wale watakaokaa viti vya
rangi ya bluu na kijani ambavyo
jumla yake ni 36,693 katika uwanja
huo wenye viti 57,558. Viingilio
vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya
rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa
VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh.
30,000.
Tiketi zitakazotumika kwenye mechi
hiyo ni za elektroniki, na zimeanza
kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka
huu). Tiketi zinapatikana kwa
mtandao wa M-PESA, CRDB
Simbanking na maduka ya CRDB
Fahari Huduma ambayo yapo zaidi
ya mia moja sehemu mbalimbali
jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo namba 27
itakayochezeshwa na mwamuzi Israel
Mujuni Nkongo akisaidiwa na John
Kanyenye na Ferdinand Chacha
itaanza saa 10 kamili jioni.
Kamishna wa mechi hiyo ni Salum
Kikwamba kutoka mkoani
Kilimanjaro.
Washabiki wanatakiwa kununua
tiketi mapema, kwani hazitauzwa
uwanjani siku ya mechi. Milango
yote ukiwemo ule wa upande wa
Mbagala (Uwanja wa Ndani)
itafunguliwa kwa ajili ya washabiki,
na itakuwa wazi kuanzia saa 4
asubuhi.
Magari maalumu tu yenye stika
ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia
uwanjani kwa kupitia Barabara ya
Mandela. Pia washabiki
hawaruhusiwi kuingia uwanjani
wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na
mabegi makubwa. Barabara ya
kuingilia upande wa Chang’ombe
itafungwa kwa watumiaji wa magari.
0 comments:
Post a Comment