Kitabu cha 2sides
cha mlinzi wa klabu ya Rio Ferdinand huenda kikawa ndicho kitabu
kinachoongelewa sana kwa sasa nchini England pengine kuliko vyote ambavyo
vimewahi kutolewa na nyota wa mchezo wa soka.
Baada ya
kukosoa mbinu za aliyekuwa kocha wake katika klabu cha Manchester United David
Moyes kwa kuziit za aibu kisha kudai kuwa wachezaji wa timu ya taifa ya England
wanalelewa kama watoto,leo hii Ferdinand amekuja na mpya baada ya kufichua kuwa
alimchukia mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Mholanzi Denis Bergkamp
kisa
tu alikataa kubadilishana nae jezi baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi
kuu kati yake Leeds United na Arsenal.
Ferdinand
amesema “Wakati mmoja,nikiwa bado kinda
nikichezea Leeds,nilimuuliza Bergkamp Unataka kubadilishana jezi baada ya
mechi?”
Akanijibu
kwa mkato “Huwa sibadilishani jezi” basi
tangu hapo nikaanza kumchukia nikaacha hata tabia ya kuomba watu
jezi.Nikagundua kwamba kuomba omba jezi kunawafanya watu wajione wako juu yako.
0 comments:
Post a Comment