Vilabu vikubwa barani Ulaya vitakutana wiki
ijayo ili kutoa ombi kwa shirikisho la soka
duniani FIFA kuandaa michuano ya dimba la
dunia nchini Qatar kati ya tarehe 28 mwezi
Aprili na 29 mwezi May .
Qatar ilikabidhiwa maandalizi ya michuano
hiyo mwaka 2010 lakini tume inayotaka
kuliandaa dimba hilo wakati wa baridi
imekuwa ikiendelea na kazi yake.
Muungano wa vilabu vya Ulaya,kikiwemo
kilabu cha Manchester,Liverpool,Barcelona na
Bayern Munich unataka kuwasilisha ombi hilo
ikiwemo kuanza mechi za ligi ya msimu wa
mwaka 2021 na 2022 wiki mbili mapema na
kucheza mechi za mwisho za kombe la FA
baada ya fainali za dimba hilo.
Huku Dimba la dunia likitarajiwa May
29,hatua hiyo itasababisha kombe la FA
nchini Uingereza kukamilika mwezi Juni.
Muungano huo unaowakilisha timu 214 za
bara Ulaya ,unaamini hilo huenda likaathiri
mashindano ya mataji ya nyumbani nchini
Ufaransa na Uhispania iwapo ombi lao
litapuuzwa.
0 comments:
Post a Comment