Kiungo Mathieu Flamini bado anaendelea kujuta kuhusu
Fabregas.Hajuti kwa kuwa Fabregas hakurudi Arsenal kama alivyofanya yeye ama
kumuona akiwa kavaa jezi za blue za klabu ya Chelsea bali anajuta kutowahi
kutwaa ubingwa wowote ule akiwa na rafiki yake huyo kipenzi.
Wote walikulia Arsenal.Wakawa na kubaki marafiki wakubwa
mpaka leo hii.Ni majirani katika jiji la London nyumba zao ziko pua na mdomo.
Lakini Flamini anaikumbuka ile miaka ya furaha wakiwa
pamoja Arsenal ambayo iliishia bila ya kumbukumbu yoyote ile ya ubingwa.
Flamini anasema
“Nilikuja hapa nikiwa na miaka
20,Fabregas alikuwa mdogo kwangu kwa miaka mitatu (3) imekuwa ni miaka kumi (10)
sasa tangu kipindi hicho.
Katika kipindi hicho tulipitia mambo mengi
pamoja.Tulikuwa kwenye fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2006.Nimekuwa
nikimpigania kwa miaka mingi.
2007 wachezaji wa Arsenal wakiwa nyumbani kwa Malkia Elizabeth |
Wakati tuko pamoja hapa tulitengeneza uelewano mkubwa
sana uwanjani.Alikuwa akishambulia sana huku mimi nikizuia sana,nikipambana kwa
ajili yake.Jumapili nakutana nae haitakuwa rahisi kumkaba kwanza ni kwa sababu
ni mchezaji mzuri na pia ni rafiki yangu kipenzi.
Natamani tungewafunga Barcelona siku ile na kutwaa
ubingwa wa Ulaya nikiwa sambamba nae ama ubingwa uliopita wa FA.Ni jambo gumu
kumuona akiwa katika jezi za blue za Chelsea,ulikuwa ni uamuzi wake kwenda
huko.Ni rafiki yangu bila kujali uamuzi aliouchukua bado nitaendelea kumuunga
mkono.
0 comments:
Post a Comment