728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 29, 2014

    MANDZUKIC:GUARDIOLA ALINIKOSEA HESHIMA

    Mshambuliaji Mario Mandzukic ameibuka na kudai kuwa aliyekuwa kocha wake katika klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola alimkosea heshima.

    Mandzukic ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Atketico Madrid katika mahojiano aliyofanya na kituo cha Sportske Novosti,na mahojiano hayo kuchapichwa na gazeti maarufu la michezo la Mundo Deportivo amesema Guardiola ndiye aliyemfanya akahama Bayern Munich baada ya kumkosea heshima na kumuona hafai.

    Mandzukic aliyejiunga na Bayern mwaka 2012 na kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 34 katika michezo 55 anasema ``Kabla ya kuja kwa Guardiola maisha chini ya Jupp Heynkes yalikuwa mazuri mno na ndiyo maana haikushangaza tulipotwaa mataji matatu"

    Lakini alipokuja Pep mambo yalianza kwenda kinyume nikawa sipangwi mara kwa mara licha ya kufanya vizuri katika nafasi chache nilizopata.Pep hakutaka hata niwe mfungaji bora wa ligi kwani licha ya magoli 18 niliyokuwa nimefunga bado aliendelea kunidharau na kuniweka benchi.

    Nakumbuka hata katika mchezo wa fainali ya DFB Pokal dhidi ya Dortmund licha ya kuwa nilikuwa fiti bado Pep hakunipanga.Siwezi kumsamehe achilia mbali kukaa naye meza moja na kunywa naye kahawa siwezi".Alimaliza Mandzukic

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MANDZUKIC:GUARDIOLA ALINIKOSEA HESHIMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top