728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 29, 2014

    MSEMO WA HE SCORES WHEN HE WANTS WAMCHANGANYA SAKHO

    Mshambuliaji matata wa klabu ya West Ham anayetesa katika ligi ya Epl Diafra Sakho (24) ametoa siri kuwa msemo wa kiingereza usemao ``He scores when he wants" ulimuacha njia panda wikendi iliyopita.

    Sakho ambaye ametua West Ham kwa kitita cha £3.5m akitokea klabu ya Metz ya Ufaransa na kufanikiwa kuwafungua wagonga nyundo hao wa jiji la London magoli saba katika michezo nane amegeuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo ambao wikendi iliyopita walipata ushindi wa kishindo baada ya kuwatandika mabingwa watetezi wa taji la Epl Manchester City kwa goli 2-1 huku goli la ushindi likifungwa na Sakho.

    Baada ya goli lile mashabiki wa West Ham wakaanza kuimba wimbo usemao ``He scores when he wants" (Anafunga anapotaka),wimbo huo ulionekana kumchanganya kutokana na kutojua maana yake.

    Sakho anasema ``Sikujui wanamaanisha nini ilinibidi nimuulize mchezaji mwenzangu Ricardo Vaz T,baada ya kunitafsiria maneno yale kwa kweli nimepata nguvu ya kuendelea kupambana ili niendelee kuwafurahisha mashabiki wangu"

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MSEMO WA HE SCORES WHEN HE WANTS WAMCHANGANYA SAKHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top