WACHEZAJI wanne wa kikosi cha Yanga
wataikosa mechi ya wikiendi hii dhidi ya
Kagera Sugar baada ya kukumbwa na
matatizo mbalimbali.
Daktari wa Yanga, Juma Sufiani,
amewataja wanne hao kuwa ni mabeki;
Nadir Haroub ‘Cannavaro na Kelvin
Yondani wanaosumbuliwa na malaria,
winga machachari Simon Msuva
anayesumbuliwa na mgongo wakati
Hussein Javu yeye ameumia goti.
Sufiani alisema kuwa Msuva aliumia
mazoezini wakati Javu aliumia goti
kwenye mechi dhidi ya Stand United
wikiendi iliyopita.
“Wote tumewaandikia mapumziko ya wiki
nzima ili waweze kupona kabisa, si
matatizo makubwa, lakini ni vyema
wakapumzika. Javu atafanyiwa vipimo
baada ya kurejea Dar ili kubaini ukubwa
wa tatizo lake,” alisema Sufiani.
Katika hatua nyingine, beki wa kulia wa
Yanga, Oscar Joshua, ameweka wazi siri
ya safu yao ya ulinzi kufanya vizuri
akisema ni namna wanavyonolewa na
kocha Marcio Maximo.
Alisema: “Ubora wa safu yetu kusema
kweli, siri ni kujituma wenyewe, lakini
pili ni kufuata maelekezo ya kocha wetu
Maximo kwani mfumo anaotufundisha wa
namna ya kuzuia, kuijenga ngome yetu
lazima ufanye kazi.
“Kocha amekuwa akitupa mbinu ambazo
ni ngumu kwa wapinzani kutupita. Kazi
hii iliimarishwa mara baada ya mechi ile
tuliyofungwa na Mtibwa. Kwa staili hii
tunayocheza, hata kama mimi sitakuwepo
au mwingine yeyote, atakayeingia
akicheza kwa maelekezo, ni ngumu
kufungwa,”alisema Oscar.
0 comments:
Post a Comment