728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 28, 2014

    BAKHRESA,BINSLUM WANAVYOTUMIA UBONGO WA KEVIN O’LEARY KUFUNGA MAGOLI MAWILI KWA SHUTI MOJA.


    “Kitu cha kwanza na muhimu kwenye
    vita ni pesa,Pesa inamaanisha vitu
    vingine vyote,Askari,bunduki na
    risasi”.Maneno ya hekima ya
    miongoni mwa wanawake majasiri
    kuwai kutokea Duniani.Ida
    Tarbell,Mwalimu na mwandishi wa
    habari za siasa wa zamani wa
    marekani.Miaka sabini sasa tangu
    Mungu amchukue,Lakini maneno yake
    yanaishi mpaka leo.Pesa ndio kila
    kitu bwana.Tafuta pesa
    kwanza,Vingine vitatengenezwa na
    pesa uliyopata.Pesa ni silaha kuu ya
    kumshinda adui yako.Hakuna kitu
    bora kinachoendeshwa bila pesa.Kwa
    ufupi Pesa ndio alama kuu ya
    mafanikio.Hata kwenye soka pesa
    inacheza zaidi kuliko miguu ya
    wachezaji.
    Mpira wa leo umetawaliwa na watu
    wenye pesa zao, Lakshmi Mittal,
    Alisher Usmanov, Roman Abramovich
    ni miongoni mwa mabilionea Duniani
    wanaomiliki na kudhamini vilabu
    mbalimbali kwenye ligi kuu ya
    England. Ligi ya uingereza inapendeza
    kutokana na mchango wa vigogo
    hawa wenye pesa zao.Bila jeuri ya
    pesa kusingekuwa na ubingwa wa
    Chelsea wala Manchester
    City.Makombe ya Chelsea
    yamenunuliwa na Pesa chafu za
    Roman Abramovich,Pesa hizo hizo
    ndio zimeleta mapinduzi ya soka
    nchini Uingereza.Ni jambo la kawaida
    sasa kuona vilabu vikongwe uingereza
    Liverpool na Manchester united
    vikitupwa mbali na mbio za
    ubingwa.Hakika pesa imetengeneza
    ligi kuu ya uingereza.
    Patrice Motsepe, Kaizer Motuang,
    Moise Chapwe, Irvin Khoza ni
    miongoni mwa wamiliki wa vilabu
    maarufu barani Afrika.Pia watu hao ni
    miongoni mwa matajiri wakubwa
    Afrika.Ukiachana na Moize Chapwe
    waliobaki watatu yaani Patrice
    Motsepe, Kaizer Motuang, Irvin Khoza
    wote wanamiliki na kudhamini vilabu
    vya nchi ya Afrika kusini.Kwanini ligi
    kuu ya Afrika kusini isiwe ligi bora
    barani Afrika?.Pesa za kina Patrice
    Motsepe, Kaizer Motuang, Irvin Khoza
    ndio chagizo kubwa ya ligi hiyo kua
    bora na yenye mvuto kwenye bara letu
    pendwa la Afrika.
    Hakika tangu kuzaliwa kwangu sijawai
    kuona ligi ya Tanzania inapendeza
    kama miaka hii miwili ya karibu.Mvuto
    wa ligi unaongezeka kadiri miaka
    inavyosonga.Ligi kuu ya mwaka jana
    ilikua nzuri kuliko ya mwaka juzi,pia
    bila shaka ya mwaka huu mpaka
    ilipofika inaelekea kunoga kuliko ya
    mwaka jana.Nyuma ya kuimalika kwa
    ligi hii kuna watu na pesa zao
    wamesimama.Wapo wengi ila leo
    napenda kuutambua mchango wa
    Bakhresa na Binslum.Kama ningekuwa
    tff ningeandaa tuzo kwa ajili ya watu
    hawa.Bakhresa na Binslum ni
    mikongoni mwa matajiri wachache
    wenye mapenzi ya dhati na mpira
    wetu.Hawa watu bila shaka wana
    malengo ya dhati kukuza soka la
    Bongo.Kaizer chief, si timu kongwe
    kama Simba na Yanga,ila ni timu bora
    kuliko simba na Yanga.Kaizer
    Motuang alipata maono ya kuanzisha
    kaizer chiefs mwaka 1970,Bakhresa
    alivyoanzisha Azam ni kama Kaizer
    alivyoanzisha Kaizer Chiefs.Mapinduzi
    ya soka la Afrika Kusini yalianzia kwa
    Kaizer chiefs kama Tanzania
    yalivyoanzia kwa bakhresa.Licha ya
    bakhresa kumiliki timu ya azam pia
    tajiri huyo ametoa udhamini kwa klabu
    zote zinazoshiriki ligi kuu Tanzania
    bara.Pesa za bakhresa
    zimehamasisha miguu ya wachezaji
    wengi wanaoshiriki ligi kuu.Pesa zake
    zimepunguza ukata uliokua
    unazikabiri timu zisizo na
    wadhamini.Hakika pesa za Bakhresa
    zinacheza ligi kuu yenye
    mvuto.Ukiachana na Bakhresa kuna
    mtu anaitwa Binslum, Binslum
    ametumia zaidi ya million 450
    kuwekeza kwenye soka.
    naye amefanya kwa sehemu
    yake.Ametoa udhamini wa vilabu
    vitatu Tanzania bara,Tena kati ya
    vilabu hivyo vitatu ,viwili ndio kwanza
    vimepanda ligi kuu msimu huu.Stand
    united na Ndanda zimepanda ligi kuu
    huku zikijihakikishia mamilioni kutoka
    kwa bakhresa na Binslum.Hii ni tofauti
    na zamani timu inapanda daraja
    inakosa hata pa kuanzia,Jambo hili
    lilipelekea timu kubwa kutumia
    udhaifu wa timu ndogo kupenyeza
    kirusi kinachoitwa rushwa.Hata kama
    Binslum na Bakhresa hawajamaliza
    tatizo la rushwa lakini watakua
    wamepunguza kwa asilimia kubwa.
    Kama kungekua na bakhresa watatu
    na binslum watano hakika ligi yetu na
    soka letu kwa ujumla lingekua mbali.
    “Hivi ndivyo nnavyofikiri kuhusu pesa
    yangu,pesa yangu ni kama
    askari,nawatuma vitani kila siku
    nataka iende ikakamate mateka na
    kuwarudisha nyumbani”.Maneno ya
    bilionea jeuri Duniani,Raia wa Canada
    Kevin O’Leary. Matajiri na Makampuni
    makubwa inabidi wajifunze kuwekeza
    na kujitangaza kupitia soka.Soka ni
    biashara nzuri,Bakhresa, Patrice
    Motsepe, Kaizer Motuang, Moise
    Chapwe na Irvin Khoza wanajua
    umuhimu wa kutumia askari pesa
    kupata mateka(faida) kwenye vita ya
    soka(biashara).Bila shaka Bakhresa
    na Binslum walimuelewa vizuri Kevin
    O’Leary.
    Licha ya Bakhresa na Binslum
    kusaidia soka letu bali pia na wao
    kuna faida wanapata kupitia
    kutangaza biashara zao.Watanzania
    wengi wanapenda soka,Bidhaa za
    Binslum na Bakhresa zinapendwa na
    watu wengi kwasababu ya kujitangaza
    kwao haswa kupitia soka. Wito wangu
    kwa matajiri na makampuni makubwa
    kuamka na kuanza kuwekeza kwenye
    soka.Uwekezaji wao kwenye soka
    utakua na faida kwa Taifa lao pia na
    kwao binafsi.Bakhresa na Binslum
    wanapiga shuti moja na kufunga
    magoli mawili,yaani wanatumia pesa
    zao kwenye soka kufunga magoli
    mawili,la kwanza wanafunga kwa soka
    la Tanzania na la pili kwenye biashara
    zao.Tusiwaache Binslum na Bakhresa
    pekee wafaidi akili za Kevin O’Leary
    kwenye vita(biashara) ya soka la
    Bongo.Tusiwaache watu hawa
    watumie peke yao ubongo wa Kevin
    O’Leary kufunga magoli mawili kwa
    shuti moja.
    Na
    Allen kaijage
    0655106767
    kaijagejr@gmai

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAKHRESA,BINSLUM WANAVYOTUMIA UBONGO WA KEVIN O’LEARY KUFUNGA MAGOLI MAWILI KWA SHUTI MOJA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top