Huenda mtu
mwenye wakati mgumu kwa sasa katika duru za soka duniani akawa ni kocha wa klabu
ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger akiwa bado hajapona maumivu ya kichapo cha
bao mbili kwa nunge toka kwa klabu ya Chelsea, ndani ya muda mfupi uliopita amepoteza
kiungo wake Mesut Ozil kutokana na majeraha ya goti.
Chama cha
soka cha Ujerumani kimesema kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid alikosa
kufanya mazoezi leo katika kambi iliyoko Frankfurt na kuelekea Munich akiwa na
daktari wa timu hiyo Hans-Wilhelm
Muller-Wolhlfahrt kufanyiwa
vipimo vya MRI vilivyobaini tatizo hilo ambalo
kupona kwake huchukua wiki 10-12.
Kufuatia
majeruhi hayo Ozil atakosa michezo miwili ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ijayo ya Ulaya
Euro 2016 dhidi ya Poland na Ireland huku akitarajiwa kuvaa tena jezi za
Arsenal mwakani.Mbali ya Ozil majeruhi wengine wanaendelea kumuadhibu Arsene
Wenger ni Olivier Giroud,Mathieu Debuchy,Theo Walcott,Aaron Ramsey,Abou Diaby
na Yaya Sanogo.
0 comments:
Post a Comment