728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 15, 2014

    PHIRI APEWE MUDA WA KUJENGA SIMBA YA MSIMU UJAO.


                “Kazi ya pamoja(Teamwork) inaleta matokeo mazuri, lakini maono hayo huwa ndoto pale kiongozi anapokuwa na malengo makubwa huku akiwa na timu isiyostahiki”.Najaribu kumuelewa John C Maxwell,Mchungaji maarufu na miongoni mwa watunzi bora wa vitabu  Marekani.Siku zote matokeo bora huletwa na timu bora.Na timu bora ni ile inayofanya kazi kwa pamoja(teamwork).lakini ili upate timu inayocheza kwa pamoja na kwa umoja lazima utengeneze kitu kinachoitwa ‘Chemistry’(kemia)
    .
                   Kwenye soka  tumekuwa tukitumia maneno kama chemistry(kemia) huku wengi tukiwa hatujui maana yake.nilishawai kutoa maana ya chemistry wakati naizungumzia Manchester ya van gaal.Nilisema  “kemia ni masomo ya atomi na mkusanyo wa atomi kuwa molyekuli.Yaani hizo atomi ukizichanganya utapata kitu kizima kinachoitwa molyekuli. ukichanganya hydrogen na oxygen unapata maji,ukichukua sodium na chlorine unapata chumvi na ukitaka kupata chumvi na maji kwa pamoja ni lazima uchanganye acid na base Mchezaji ndio atomi yenyewe na timu ndio molyekuli.

    Kitendo cha kuwaunganisha wachezaji katika timu moja na wachezaji hao kuungana katika mfumo husika ndio tunaita chemistry(kemia).Kocha anaposhindwa kupata wachezaji husika kwenye mfumo husika hapo ndipo tunasema kashindwa kutengeneza chemistry kwenye timu.Na kushindwa kupata ‘chemistry’ kwenye timu ndiko kunakofanya timu isicheze kwa maelewano na hapo ndipo tunapokosa teamwork”.

                   Na hili ndio tatizo kubwa linaloikabili Simba.’Chemistry’ ndio inafanya simba isicheze kwa maelewano.Mechi iliyopita Dhidi ya stand united kikosi cha simba kwenye sehemu ya ulinzi kulikua na wachezaji watano ambao hawajai cheza mechi kwa pamoja,Kiufupi wachezaji wote watano huu ndio msimu wao wa kwanza kucheza simba kwenye ligi kuu,Ukiachana na kipa ‘Cassilas’,Mohamed Hussein,Mugeveke,Isihaka na Miraji ndio ilikua mechi yao ya kwanza kucheza kwa pamoja.Licha ya umri mdogo na kukosa uzoefu kwenye ligi bado mawasiliano yalikua tatizo kubwa kwao,Utaona  kabisa atomi hizi zilishindwa kutengeneza molekyuli ya kueleweka.

    Kama uliwaangalia vizuri kila mtu alikua akicheza anavyojua yeye na si kama timu inavyotakiwa icheze,Tatizo hili lilionekana haswa kwa mabeki wa kati,nawazungumzia Mugeveke na Isihaka.Kama Stand united wangekua na mshambuliaji anayejua kulazimisha mashambulizi kama Danny Mrwanda alivyokua akifanya kwenye mechi dhidi ya Simba basi bila shaka Stand united wangeondoka na ushindi.

                  Ukiacha Safu ya ulinzi kwenye kiungo pia kuna tatizo hilo hilo la kukosa muunganiko au maelewano kwa lugha nyepesi.Kwizera,Mkude na kisiga ni miongoni wa viungo bora kabisa kwenye ligi kuu Tanzania.Kama ni vipaji hakika Mungu amewapa ,lakini mpaka sasa hawa watu wameshindwa kucheza pamoja kama timu.Kwizera,Kisiga na Mkude ndio mara yao ya kwanza kucheza kwa pamoja kwenye timu moja.Kwa haraka utagundua vipaji hivi maridhawa vimekosa kitu kinachoitwa “Chemistry”.

                  Nikimuangalia Emmanuel Okwi uwanjani namkumbuka Michael Jordan,Michael Jordan ambaye inasemekana ni mchezaji bora wa kikapu kuwai kutokea ulimwenguni,Jordan kila timu anayoichezea macho yote walikua wakimuangalia yeye.Jordan alikuwa akijitahidi kwa hali na mali timu ishinde lakini mara nyingine timu anayoichezea inapata matokeo mabaya yanayopelekea kukosa kombe.

    Jordan alikua akiumia sana na siku moja ilibidi avunje ukimya na akasema maneno haya “Kipaji kinaweza kushinda mechi,lakini akili na kufanya kazi kwa pamoja ndipo kunashinda kombe”.Ukiangalia jitihada anazofanya okwi uwanjani ni kama wamemsusia timu.Hapati ushirikiano unaohitajika kutoka kwa wachezaji wenzake,Mpaka sasa Simba imefunga magoli 4 hakuna hata goli moja lisilomuhusisha Okwi.Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua washambuliaji wa simba wamekosa ‘combination’,Hapo  ndipo tunarudi kule kule kwenye “Chemistry”

                  Kabla ya msimu huu kuanza simba ilitema wachezaji zaidi ya 11,Wachezaji 11 ni wengi sana,ni sawa na kikosi kamili uwanjani.Ukichukua maamuzi magumu ya kutema wachezaji 11 kwenye timu kwa msimu mmoja maana yake unataka kujenga timu upya.Simba wana wachezaji  wengi wapya ,pia wana kocha mpya,Japo inawezekana lakini si rahisi kwao kupata kombe kwa msimu huu huku wakiwa na kila kitu kipya,Kipa na mabeki wageni,Viungo na washambuliaji  wapya.

                 Simba chini ya kocha Phiri inabidi wapewe muda wa kujenga timu imara ya misimu ijayo,Kupata “Chemistry” kwenye timu kunahitaji muda wa kutosha.Simba inabidi impe uhuru kocha Phiri msimu mzima ,huku wakimuhakikishia kibarua chake ili afanye kazi ya kujenga timu bila presha yeyote.Wapenzi na wadau simba inabidi wakubali kuupoteza msimu huu kwa ajili ya misimu bora ijayo.Simba kwa kikosi hichi walichonacho kina wachezaji wengi sana wenye vipaji.Nafikiri baada ya msimu huu Simba watakua wameshapata “chemistry” ,nafikiri phiri atakua ameshachanganya atomi zake vizuri na kupata molekyuli imara.Nina imani Simba wakifanya hivi watarudi tena kama timu ya kuogopwa Afrika mashariki na kati.
                                                                      Na allen kaijage
                                                                 kaijagejr@gmail.com
                                                                         0655106767

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PHIRI APEWE MUDA WA KUJENGA SIMBA YA MSIMU UJAO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top