Sao Paulo,Brazil.
CHAMA cha soka cha Brazil (CBF) kimetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu wa timu yake ya taifa Carlos Caetano Bledorn
Verri Dunga
Dunga,52,mshindi wa kombe la dunia la mwaka 1994 nchini Marekani ameondolewa katika wadhifa huo baada ya Jumatatu alfajiri Brazil kutupwa nje ya michuano ya Copa America Centenario kufuatia kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Peru.
Mbali ya Dunga,aliyekuwa msaidizi wake,Gilmar Rinaldi na wengine pia nao wametupiwa virago.
Hii ni mara ya pili kwa Dunga kukumbwa na kadhia hiyo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2010 baada ya Brazil kuondolewa katika hatua ya makundi ya kombe la dunia lililofanyika Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment