Leonardo Bonucci
Musona:Mabinga wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Yanga SC wameripotiwa kumsajili mshambuliaji Walter Musona,24,kutoka FC Platinums ya Zimbabwe kwa mkataba wa miaka miwili.(Bingwa)
Gomes:Chelsea imekwaa kisiki katika mbio zake za kutaka kuinasa saini ya kiungo wa Valencia Mreno Andre Gomes,22, hii ni baada ya ofa yake ya £32m kutupiliwa mbali na miamba hiyo ya Mestalla.Valencia inang'ang'ania ipewe £42m ili iweze kumalizana na Benfica ambayo ina haki ya kupata 25% katika mauzo hayo. (SSN HQ)
Bonucci:Vilabu vya Chelsea na Man City kwa pamoja vimeonyesha kuvutiwa na mlinzi wa kati wa Juventus,Leonardo Bonucci,29.Taarifa zaidi kutoka Italia zinasema Juventus haitaki kumwachia staa wake huyo lakini ikibidi basi vilabu vinavyomtaka vitalazimika kutoa kitita cha €60m. (Corriere dello Sport)
Mandanda:Chelsea imefungua mazungumzo na kipa wa Marseille, Mfaransa Steve Mandanda ili kuangalia uwezekano wa kumsajili pindi mkataba wake utakapokwisha mwishoni mwa mwezi ujao. Mandanda, 31 anatazamwa kama mtu sahihi wa kuja kumpa changamoto kipa namba moja wa klabu hiyo Thibaut Courtois,23.(Guardian)
Wijnaldum:Roma inakaribia kuinasa saini ya kiungo wa Newcastle United Mholanzi ,Georginio Wijnaldum,24,hii ni baada ya vilabu hivyo viwili kuwa karibu kuafikiana dau la €15m.(La
Gazzetta dello Sport)
Babacar:Crystal Palace inameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa
Fiorentina Msenegal,Khouma Babacar.Kutoka Italia taarifa zinasema staa huyo mwenye miaka 23 anaweza kuhama kwa ada ya €9m licha ya kuwa na mkataba mpaka mwaka 2019.
Pedro:Winga wa Chelsea Muhispania Pedro Rodriquez,28, amedai kufanya mazungumzo na mabosi wa Barcelona na amekiri kutamani kutaka kurejea Nou Camp kwa mara nyingine.(BeIN)
0 comments:
Post a Comment