Dar es Salaam,Tanzania.
KATIKA kuhakikisha inaimarisha safu yake ya ushambuliaji, uongozi wa
klabu ya Yanga umefanikiwa kumalizana na straika kutoka FC Platinum ya
Zimbambwe, Walter Musona, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Walter ni mchezaji aliyependekezwa na kiungo na straika wa timu hiyo,
Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambao wamecheza naye muda mrefu
wakijua uwezo wake ndani ya uwanja.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zinadai kwamba straika huyo
alitakiwa kuwasili wiki mbili zilizopita ikashindikana lakini sasa
mambo yanakwenda sawa.
Kuchelewa huko kulitokana na Yanga kutafuta njia nzuri za kuachana na
Mniger Boubakar Issouf, ambaye ameshindwa kuendana na kasi ya
Wanajangwani hao lakini sasa taarifa zinadai kuwa kila kitu kimekwenda
sawa.
“Sasa kila kitu kinaenda vizuri baada ya kumaliza mchakato wa kulipwa
haki zake Mniger pamoja na uchanguzi, Musona anatua wakati wowote na
kusaini mkataba wa miaka miwili,” alisema kigogo mmoja kutoka Yanga.
Kigogo huyo alisema baada ya kusaini mkataba ataungana na wachezaji
wenzake nchini Uturuki kwa ajili ya kambi kujiandaa na mchezo wao dhidi
ya Mo Bejaia ya Algeria.
Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano, Jerry Muro,
alithibitisha kuwepo kwa mazungumzo na mchezaji huyo na kuwahakikishia
Wanayanga kuwa angetua nchini muda wowote.
CHANZO:DIMBA
0 comments:
Post a Comment