Lille,Ufaransa.
SLOVAKIA imefufua matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 baada ya kuifunga Urusi kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa kundi B uliochezwa mchana wa leo katika uwanja wa Pierre-Mauroy stadium huko jijini Lille.
Mabao ya Slovakia yamefungwa na Vladimir Weiss dakika ya 32 huku lile la pili likifungwa na Marek Hamsik dakika ya 45.Bao la Urusi limefungwa kwa kichwa dakika ya 80 na Denis Glushakov.
VIKOSI
RUS: Akinfeev; Schennikov, Ignashevich,V.Berezutski, Smolnikov; Smolov, Neustadter,Golovin, Shatov, Kokorin; Dzyuba
SVK: Kozacik; Pekarik, Skrtel, Durica,Hubocan; Mak, Kucka, Pecovsky, Hamsik,Weiss; Duda
0 comments:
Post a Comment