728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 15, 2016

    SHOMARI KAPOMBE MCHEZAJI BORA WA MWAKA AZAM FC

    Dar es Salaam,Tanzania.

    BEKI mahiri wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, amechaguliwa na mashabiki kuwa Mchezaji Bora wa timu hiyo msimu uliopita.

    Zoezi la kumtafuta mchezaji wa kutwaa tuzo hiyo lilianza rasmi Juni 8 mwaka huu kwa hatua ya awali kabla ya Ijumaa iliyopita kuingia hatua ya fainali iliyohusisha wachezaji sita waliopigiwa kura nyingi zaidi na mashabiki katika akaunti ya Azam FC kwenye mtandao wa kijamii wa facebook.

    Hadi zoezi hilo linahitimika leo Jumatano saa 6.00 mchana, Kapombe amewabwaga wapinzani wenzake watano kwenye kinyang’anyiro hicho ambao ni Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, beki kisiki Pascal Wawa, kipa Aishi Manula na mawinga Farid Mussa na Ramadhan Singano ‘Messi’.

    Beki huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kujizolea kura 203 kati ya zote 560
    zilizokubaliwa, Aishi amemfuatia akiwa nazo 125, Farid (95), Singano (48), Himid (45) na Wawa (44).

    Jumla ya kura 710 zilipigwa na mashabiki mbalimbali walioshiriki zoezi hilo, lakini ni 560 tu zilizokubaliwa, nyingine 150 ziliharibika baada ya wapigaji kukiuka masharti kwa wengine kupiga kura zaidi ya moja na baadhi yao kuwapigia kura wachezaji wawili tofauti huku zingine zilizokataliwa zikiwa ni kwa wale waliokosea majina.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SHOMARI KAPOMBE MCHEZAJI BORA WA MWAKA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top