728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMANNE YA LEO JUNI 14,2016.

    Luis Nani.

    Nani:Ndoto ya mashabiki wa Manchester United kumuona tena winga wao wa zamani Mreno Luis Nani,28, akirejea Old Trafford imefutika baada ya staa huyo wa Fenerbahce kukubali kujiunga na Inter Milan ya Italia kwa kandarasi ya miaka mitatu.(Record)

    Mkhitaryan:Borussia Dortmund imechoka kuvutana na staa wake wa kiungo Muarmenia Henrikh Mkhitaryan,26, kuhusu kusaini mkataba mpya.Taarifa kutoka Ujerumani zinasema Borussia Dortmund imempa staa huyo wa zamani wa Shaktar Donestik mpaka wikendi hii kuamua kama anaondoka ama anabaki klabuni hapo.(London Evening Standard) Blick

    Mahrez:Leicester City imeripotiwa kuwa itahitaji kupewa malipo ya £30m kama ada ya uhamisho ikiwa winga wake Mualgeria Riyad Mahrez,25, ataomba kuondoka msimu huu.(The Sun)

    Umtiti:Beki wa Olympique Lyonnais Mfaransa Samuel Umtiti amekubali kujiunga na Barcelona kilichobaki ni vilabu hivyo viwili kukaa mezani na kufikia makubaliano.Umtiti,22,anakadiliwa kuwa na thamani ya €30m.(Le Dauphine)

    Sane:Schalke 04 kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Michezo Christian Heidel imekanusha uvumi ulionea siku ya Jumatatu kuwa imekubali kumuuuza staa wake wa safu ya kiungo Leroy Sane,20, kwenda Manchester City kwa day la £40m.(Bild)

    Dahoud:Liverpool imekwaa kisiki katika mbio zake za kutaka kumsajili kiungo Mjerumani Mahmoud Dahoud baada ya klabu yake ya Borussia Monchengladbach kukataa kumuuza.Monchengladbach imemtaka Dahoud,20,abaki kwa msimu mmoja zaidi na kisha itamruhusu kuondoka msimu ujao.(Goal)

    Slimani:Vilabu vya Liverpool na Arsenal vimeangukia pua baada ya Sporting Lisbon kukataa ofa ya £20m kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake Mualgeria Islam Slimani,24.Taarifa zaidi zinasema Liverpool na Arsenal zinaweza kumpataa staa huyo wa Algeria ikiwa tu zitakuwa tayari kutoa kitita cha £24m.Msimu uliopita Slimani aliifungia Sporting Lisbon mabao 30 katika michezo 38.(Noticias ao Minuto)

    Sigurdsson:Leicester City inataka kutisha zaidi msimu ujao na katika kutaka kuona hilo linafanikiwa tayari imefungua mazungumzo na Swansea City ili kuangalia uwezekano wa kumsajili staa wa klabu hiyo Muiceland,Gylfi Sigurdsson. Msimu uliopita Sigurdsson,28,aliifungia Swansea City mabao 11 katika michezo 36.(Tutto Mercato)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA JUMANNE YA LEO JUNI 14,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top