728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 14, 2016

    KAZI IPO EPL MSIMU UJAO:WESTHAM UNITED YACHOMOA MMOJA VALENCIA

    London,England.

    KLABU ya West Ham United imefanikiwa kumsajili aliyekuwa winga wa Valencia,Mualgeria Sofiane Feghouli akiwa kama mchezaji huru.

    Feghouli,26,aliyekuwa kuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu wa Valencia kwa misimu kadhaa amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuwatumikia wababe hao wa London baada ya kukataa ofa ya kubaki katika dimba la Mestalla.


    Msimu uliopita Feghouli aliichezea Valencia michezo 29 ya La Liga akifanikiwa kupachika mabao manne na kutengeneza mengine mawili.

    Feghouli amekuwa mchezaji wa pili kunyakuliwa na Westham United tangu kufungwa kwa pazia la Ligi Kuu England hapo Mwezi Mei.Wa kwanza alikuwa ni kiungo mkabaji Havard Nordtveit kutoka Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KAZI IPO EPL MSIMU UJAO:WESTHAM UNITED YACHOMOA MMOJA VALENCIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top