Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm,
amewaangalia wachezaji wapya wa kikosi hicho na kutamka kuwa bado wanaendelea
kusoma mazingira, akasisitiza kuwa, wanabadilika taratibu na wakizoea mazingira
kwa asilimia mia, watakuwa moto na kuwezesha kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kocha huyo amefunguka hayo, baada ya
kuulizwa juu ya wachezaji wake wake wa kigeni katika kikosi hicho. Yanga
imesajili Wazimbabwe wawili, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ‘Ras’ na beki
kutoka Togo, Vincent Bossou.
Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya
Ghana, alisema wachezaji wake wa kimataifa tayari wameanza kuwa fiti, lakini
wakizoea mazingira ya Bongo watakuwa katika kiwango kikubwa zaidi na kuwa
msaada mkubwa kwa klabu yake inayojiandaa kushiriki michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika.
“Siwezi kumchambua mchezaji mmojammoja
lakini kama hawa wachezaji wa kimataifa wapya wakirekebisha yale makosa machache
na wakaelewa vyema, basi watakuwa na msaada katika timu mbeleni,” alisema
Pluijm.
Ikumbukwe kuwa, Yanga ipo katika maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, Agosti 22, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment