Lubumbashi,Congo.
TP MAZEMBE ikiwa nyumbani Lubumbashi katika dimba lake la Stade de Mazembe imeitambia Medeama FC ya Ghana baada ya kuichapa kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa Kundi A wa kombe la shirikisho uliochezwa jioni ya leo.
Wageni Medeama FC ndiyo waliokuwa wa kwanza kuliona lango la wenyeji wao baada ya Malik Akowuah kufunga bao la kuongoza dakika ya 2 tu ya mchezo.
Kuingia kwa bao hilo la mapema kuliwaamsha wenyeji TP Mazembe ambao walikuja juu na kumfanya kipa wa Medeama FC,Muntari Tagoe awe na kazi ya ziada ya kuokoa michomo ya hatari kadri muda ulivyokuwa ukienda mbele.
Rainford Kalaba alifanikiwa kumzidi maarifa Muntari Tagoe na kuifungia TP Mazembe bao la kusawazisha dakika ya 16' kisha kuongeza jingine dakika ya 70'.Bao jingine limefungwa na Salif Coulibaly dakika ya 45'.
0 comments:
Post a Comment