Yohan Blake, Usain Bolt, Asafa Powell na
Nickel Ashmeade wakishangilia ushindi wa mita 400
Rio de Janeiro,Brazil.
IKIWA imepita siku moja tu tangu atwae medali ya dhahabu katika mbio za mita 200 wanaume,Usain Bolt,ameweka tena rekodi nyingine baada ya alfajiri ya leo kuiongoza Jamaica kutwaa medali ya dhahà bu katika mbio za mita 400 kupokezana vijiti.
Hiyo inakuwa ni medali ya tatu ya dhahabu kwa Bolt kushinda katika michuano ya Olimpiki ya mwaka huu.Kabla ya hapo alikuwa ameshinda dhahabu katika mbio za mita 100 na 200.
Jumla Bolt ameshinda medali tisa za dhahabu katika michuano mitatu tofauti ya Olimpiki.Mwaka 2008,2012 na 2016 katika miaka yote hiyo ameshinda medali tatu tatu.Anakuwa mwanariadha wa kwanza wa mbio fupi kuwahi kutwaa dhahabu tatu katika michuano mitatu tofauti.
Michuano ya Olyimpiki ya mwaka huu imekuwa ya mwisho kwa Bolt hii ni baada ya mapema kutangaza kuwa atastaafu mchezo wa riadha mwakani mara baada ya michuano ya dunia (World Championships) huko London.
0 comments:
Post a Comment