728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 20, 2016

    UJERUMANI MABINGWA SOKA LA WANAWAKE OLIMPIKI


    Rio de Janeiro,Brazil.

    TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Ujerumani imehitimisha vyema michuano ya Olimpiki baada ya Ijumaa usiku kutwaa medali ya dhahabu kufuatia kuitungua Sweden kwa mabao 2-1 katika mchezo wa finali uliochezwa katika uwanja wa Maracana,Brazil.

    Mabao yaliyoipa ushindi huo wa kwanza wa kihistoria Ujerumani yamefungwa na Dzsenifer Marozsan na Linda Sembrant aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.Bao la kufuatia machozi la Sweden limefungwa na Stina Blackstenius.

    Ujerumani ilitinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Canada huku Sweden ikiwatoa wenyeji Brazil katika hatua ya nusu fainali.

    Katika mchezo mwingine ambao ulikuwa maalumu wa kusaka mshindi wa tatu na wanne,Canada imetwaa medali ya shaba baada ya kuwafunga wenyeji Brazil kwa mabao 2-1.









    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UJERUMANI MABINGWA SOKA LA WANAWAKE OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top