Etienne, Ufaransa.
URENO imezianza fainali za Ulaya za 2016 kwa kasi ndogo baada ya usiku wa leo kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Iceland katika mchezo mkali wa Kundi F liochezwa huko Stade Geoffroy-Guichard,Saint Etienne na kuhudhurio wa watazamani 38,742.
Ureno ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 31 tu ya mchezo baada ya Luis Nani kufunga kwa mkwaju wa chini chini akiunganisha krosi ya Andre Gomes toka wingi ya kulia.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Iceland ambao walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 kupitia kwa Birkir Bjarnason.
Ureno watarejea tena dimbani siku ya Jumamosi kuvaana na Austria huko Paris huku Iceland wao wakisafiri mpaka Marseille kwenda kucheza na Hungary .
0 comments:
Post a Comment