728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 03, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA SOKA JIONI HII YA LEO IJUMAA JUNI 3,2016

    Kpah Sherman

    KLABU ya Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini imemtupia virago aliyekuwa mshambuliaji wake Mliberia, Kpah Sherman,24,baada ya kushindwa kuifunga bao hata moja tangu imsajili mwaka mmoja uliopita kutoka Yanga SC ya Tanzania.(Binzubery)

    Koscielny:Arsenal imeiambia Manchester United kuachana kabisa na mpango wa kutaka kumsajili mlinzi wake wa kati Mfaransa Laurent
    Koscielny,30.Wakati huohuo taarifa toka Ufaransa zinasema nyota huyo wa zamani wa Lorient havutiwi kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford.(Le 10 Sport)

    Benteke:Chelsea imeripotiwa kumuweka katika mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke ikiwa itashindwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku.(The Times)

    Candreva:Chelsea imeripitowa kuandaa kitita cha €21m ili kumnasa winga wa Lazio Muitaliano Antonio Candreva, 29.Lakini taarifa kutoka Italia zinasema Lazio haitamuuza staa huyo aliyefunga mabao 12 msimu uliopita kwa ada ya chini ya €25m.(Il Tempo).

    Sambou:Everton imemsajili kwa mkataba wa miaka mitatu mshambuliaji kinda, Bassala Sambou kutoka Coventry City.Msimu uliopita Sambou,18,mzaliwa wa Ujerumani alivifungia vikosi vya vijana vya Coventry City vya U18 na 21 mabao 25.(Metro)

    Wenger: Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis amesema klabu hiyo ina mpango wa kumpa mkataba wa muda mrefu kocha wake mkuu Arsene Wenger.Gavidis,amesisitiza kocha huyo mwenye miaka 66,ameonyesha maendeleo mazuri klabuni hapo.

    Depay:Winga wa Manchester United Mholanzi Memphis Depay ameripotiwa kuwa na hofu kubwa ya kuuzwa baada ya kocha mpya wa klabu hiyo Mreno Jose Mourinho kuwa na mpango wa kufanya usajili mkubwa.( Sun )

    Blanc:PSG imeripotiwa kuwa katika mpango wa kumtupia virago kocha wake mkuu Laurent Blanc na kuwaajiri makocha Diego Simeone ama Manuel Pellegrini hii ni baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi kuwa na mpango wa kukifanyia marekebisho makubwa kikosi hicho cha Parc des Prince.(Le Parisien)

    Skrtel:Besiktas ina matumaini ya kufanikiwa kumsajili mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel kwa ada ya £7m hii ni baada ya mlinzi huyo wa Slovakia kuonyesha nia ya kutaka kuondoka kutokana na kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha kocha Jurgen Klopp.(The Sun)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA SOKA JIONI HII YA LEO IJUMAA JUNI 3,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top