Mabingwa wa Ligi Kuu nchini England Klabu ya Leicester City leo imekamilisha usajili wa mlinda mlango Ron-Robert Zieler kutoka Hannover 96 ya Ujerumani kwa ada ya Paundi Milioni 3.
Zieler, 27,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia miamba hiyo ya King Power Stadium.Mkataba huo utafikia tamati yake Juni 30, 2020.
Zieler ameichezea Hannover 96 zaidi ya michezo 200 kwa kipindi cha miaka mitano alichoichezea miamba hiyo ya Bundesliga.Pia Zieler alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Kabla ya kutua Hannover 96,Zieler alihudumu katika kikosi cha vijana cha Manchester United akiwa na akina Danny Drinkwater, Danny Simpson, Matty James na Ritchie De Laet kabla ya kutimka mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment