Berlin, Ujerumani.
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon,Pierre-Emerick Aubameyang amechaguliwa na chama cha wanasoka wa Ujerumani (VDV) kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi daraja la kwanza nchini nchini humo maarufu kama Bundesliga.
Aubameyang,26,ambaye Januari mwaka huu alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika,ameibuka mshindi kwa kumshinda mpinzani wake wa karibu Robert Lewandowski wa Bayern Munich kwa tofauti ya kura asilimia 0.2.
Aubameyang amepata asilimia 19.7 ya kura zote zilizopigwa huku Lewandowski akipata 19.5 na kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika Ligi ya Bundesliga.
Nafasi ya tatu imekwenda kwa Henrikh Mkhitaryan wa Borussia Dortmund aliyepata asilimia 12.6 ya kura zote.
Aubameyang ametwaa tuzo hiyo baada ya kuifungia Borussia Dortmund mabao 25 katika michezo 31huku pia akitoa pasi sita zilizozaa bao.
Aubameyang, Lewandowski na Mkhitaryan pia wamejumuishwa kwenye kikosi cha mwaka cha Bundesliga.
KIKOSI CHA MWAKA CHA BUNDESLIGA
Kipa: Manuel Neuer (Bayern Munich)
Mabeki: Mats Hummels (Bayern Munich), Jerome Boateng (Bayern Munich),David Alaba (Bayern Munich), Philipp Lahm (Bayern Munich)
Viungo: Thomas Müller (Bayern Munich), Henrikh Mkhitaryan (Dortmund),
Douglas Costa (Bayern Munich), Arturo Vidal (Bayern Munich)
Washambuliaji: Robert Lewandowski (Bayern Munich), Pierre-Emerick Aubameyang (Dortmund)
0 comments:
Post a Comment