Nouakchott,Mauritania.
TIMU ya taifa ya Cameroon imekuwa nchi ya tatu kufuzu Fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika AFCON 2017 baada ya Ijumaa usiku kupata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Mauritania katika mchezo mkali wa kufuzu wa kundi M huko Nouakchott,Mauritania.
Bao lililoipeleka Cameroon katika fainali hizo zitakazopigwa huko Gabon mwakani limefungwa kwa mkwaju dakika ya 29 na kiungo wake Edgar Salli.
Kwa ushindi huo Cameroon sasa wanaungana na mataifa ya Algeria, Morocco na wenyeji Gabon kujihakikishianafasi ya kucheza AFCON mwakani.
0 comments:
Post a Comment