KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Mzambia Obrey Chirwa amendoka Alfajiri ya leo kwenda Algeria kuungana na timu yake mpya, Yanga SC baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili jana kwa dau la dola 120,000 (Tsh Milioni 240) akitolea FC Platinum ya Zimbabwe.
Chirwa aliwasili jioni ya jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na muda mfupi baadaye akasaini Mkataba wa miaka miwili.
Mara moja Yanga ilituma jina lake makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika siku ya mwisho ya usajili mdogo wa mashindano ya Afrika.
Yanga wanatarajia kupata leseni yake na CAF kuanzia leo jioni ili kukamilisha idadi ya wachezaji watano wapya, baada ya wazawa kipa Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Andrew Vincent na kiungo Juma Mahadhi.
Akiwa na FC Platinums msimu huu Chirwa alifanikiwa kufunga mabao matano katika michezo minane ya Ligi Kuu ya Zimbabwe maarufu kama Zimbabwe Castle Lager Premiership.
0 comments:
Post a Comment