NEW JERSEY,MAREKANI.
COLOMBIA imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kuifunga Peru kwa penati 4-2 katika mchezo mkali wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa MetLife Stadium mjini New Jersey.
Timu hizo zililazimika kutumia changamoto ya mikwaju kuamua mshindi baada ya mbabe kushindwa kupatikana ndani ya dakika 90 za kawaida.
Penati za Colombia zimefungwa na James Rodriguez, Juan Cuadrado,Dayro Moreno na Sabastian Perez.Penati za Peru zimefungwa na Raul Ruidiaz, Renato Tapia huku penati ya Miguel Trauco ikichezwa na kipa wa Colombia David Ospina na penati ya Christian Cueva ikitoka nje la lango.
Ushindi huo umeifanya Colombia ifuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004 na inatarajiwa kukutana na mshindi kati ya Mexico na Chile. Marekani ambayo walikuwa wa kwanza kufuzu nusu fainali wao watacheza na mshindi kati ya Argentina au Venezuela.
0 comments:
Post a Comment