Paris,Ufaransa.
LIGI ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora mtoano inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo Jumanne saa 4:45 usiku kwa michezo miwili ya mkondo wa kwanza kuchezwa katika miji ya Paris (Ufaransa) na Benfica (Ureno).
Katika mchezo wa kwanza miamba wa Hispania Barcelona wao watakuwa wageni wa Paris Saint Germain huko Parc des Princes huku Borussia Dortmund wakisafiri mpaka Ureno kwenda kuvaana na Benfica
Kesho Jumatano michezo mingine miwili pia itachezwa ambapo mabingwa watetezi,Real Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kuwaalika Napoli.Bayern Munich watakuwa Allianz Arenal kupepetana na Arsenal.
Michezo mingine minne iliyosalia itachezwa wiki ijayo kabla ya kuanza kwa michezo ya mkondo wa pili.
Ratiba ya michezo ya mkondo wa kwanza
Jumanne Februari 14
Benfica v Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain v Barcelona
Jumatano, Februari 15
Bayern Munich v Arsenal
Real Madrid v Napoli
Jumanne Februari 21
Bayer Leverkusen v Atletico Madrid
Manchester City v Monaco
Jumatano, Februari 22
Porto v Juventus
Sevilla v Leicester City
Ratiba ya michezo ya mkondo wa pili
Jumanne Machi 7
Arsenal v Bayern Munich
Napoli v Real Madrid
Jumatano Machi 8
Borussia Dortmund v Benfica
Barcelona v Paris Saint-Germain
Jumanne Machi 14
Juventus v Porto
Leicester City v Sevilla
Jumanne Machi 15
Atletico Madrid v Bayer Leverkusen
Monaco v Manchester City
0 comments:
Post a Comment