Na Faridi Miraji.
Gabriel Jesus na Jack Wilshere wote jana usiku walilazimika kutoka nje ya dimba kwasababu ya majeraha kwenye kipindi cha kwanza cha mechi ya Bournemouth dhidi ya Manchester City.
Straika wa Brazil, Jesus ameshafunga mara tatu tangu atue City mwezi uliopita aliunga chini akishika mguu wake akiwa kwenye harakati za kukimbiza pasi ya Raheem Sterling kwenye pembe ya penati boksi.
Kabla ya hapo Jesus alionekana kuumia baada ya kufanyiwa faulo na beki wa Bournemouth Simon Francis na nafasi yake kuchukuliwa na Sergio Aguero katika dakika ya 13.
Na kocha wa Man City Pep Gaurdiola amesema kwamba atakuwa anasali ili kupata majibu jeraha la nyota wake sio kubwa sana.
"Kesho asubuhi ( leo ) nitapata majibu kuhusu kiwango cha jeraha la jesus, na tuna bahati mbaya sana."
"Bila shaka usiku huu (jana) nitakuwa nasali ili jeraha lake lisiwe kubwa sana."
Wilshere,pia alitoka nje ya dimba kabla ya filimbi ya mapumziko ya kipindi cha kwanza kwa jeraha la kifundo cha mguu. kiungo huyo aliumia kifundo cha mguu baada ya kuzuia vibaya shuti lililopigwa na David Silva na nafasi yaek kuchukuliwa na Benik Afobe.
0 comments:
Post a Comment