Uyo,Nigeria.
TAIFA STARS imehitimisha safari yake ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON kichwa chini baada ya usiku huu kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Nigeria katika mchezo mkali wa kundi G uliochezwa katika uwanja wa Akwa Ibam huko Uyo,Nigeria.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 77 na Kelechi Iheanacho kwa mkwaju Mkali wa mita 25.
Nyota wa mchezo wa leo kwa upande wa Taifa Stars alikuwa ni Mlinda Mlango,Aishi Manula,ambaye aliokoa michomo mingi ya hatari iliyokuwa inaelekea wavuni kwake.
VIKOSI
Nigeria XI vs Tanzania: Ikeme; Mohammed,Balogun, Troost-Ekong, Echiejile; Mikel, Onazi;Musa, Moses, Iheanacho; Ighalo
Tanzania XI vs Nigeria: Aishi, Kapombe,Hussein, V. Andrew, Mwantika, Himid Mao,Kichuya, Mkude, Msuva, Samatta, Bocco
0 comments:
Post a Comment