Mwanza,Tanzania.
LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea tena leo kwa michezo minne ya mzunguko wa tatu kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Mbeya City ikiwa ugenini CCM Kirumba imechomoza na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Mbao FC.Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Raphael Daudi,Omary Ramadhani na Ramadhani Chombo Redondo.Bao la Mbao FC limefungwa na Vincent.
JKT Ruvu ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini imetoka sare ya bila kufungana na African Lyon.
Kagera Sugar ikiwa nyumbani imeichapa Mwadui FC bao1-0.Majimaji imefungwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar.Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Salim Bonde na Rashid Mandawa.
0 comments:
Post a Comment