728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 16, 2016

    BAADA YA KUDAIWA KUTAKA KUIPIGA BEI LIVERPOOL,FSG WAJIBU MAPIGO

    Liverpool,England.

    WAMILIKI wa klabu ya Liverpool, kampuni ya Fenway Sports Group (FSG) ya Marekani,wakiongozwa na John W. Henry, wamekanusha vikali habari zilizoenea kuwa wako katika mazungumzo ya kutaka kuiuza klabu hiyo kwa wawekezaji wa Kichina kampuni ya Sino Fortune.

    Kauli hiyo ya John W. Henry imekuja baada ya jana Jumatano gazeti la The Independent la nchini England kuripoti kuwa kampuni ya FSG imepokea ofa ya Paundi milioni 700 kutoka kampuni ya SinoFortune ili kuiuza klabu hiyo yenye makazi yake Anfield.

    Kwa mujibu wa habari toka mtandao wa Liverpool Echo , ni kwamba mabosi wa FSG
    wamekana kufanya mazungumzo na kampuni hiyo toka China na kusisitiza kuwa hawana mpango wa kuiuza klabu hiyo waliyoanza kuimiliki mwaka 2010.

    Kampuni ya SinoFortune yenye ukaribu mkubwa na serikali ya China imedaiwa kuwa tayari imeshawekeza jumla ya Paundi bilioni 5.2 katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini England na mpango wake unaofuata ni kuinunua Liverpool.

    Mbali ya kuinunua Liverpool, SinoFortune pia imeripotiwa kuwa mpango wa kuvifanyia marekebisho makubwa viwanja vya Anfield na kile cha Melwood ambacho hutumika kufanyia mazoezi.Mpango mwingine ni kujenga shule (Akademi) nyingi za soka nchini China ambazo zote zitakuwa chini ya Liverpool.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUDAIWA KUTAKA KUIPIGA BEI LIVERPOOL,FSG WAJIBU MAPIGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top