728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 16, 2016

    PAYET AKARIBIA KUIVUNJA REKODI YA ZIDANE UFARANSA

    Paris,Ufaransa.

    BILA shaka Dimitri Payet kwasasa ndiye mchezaji anayeongelewa zaidi katika kikosi cha Ufaransa kinachopambana kuuwania Uchampioni wa Ulaya (Euro) baada ya kuukosa kwa miaka mingi sasa.

    Payet,28, ambaye tayari ameshaanza kupigiwa chapuo kuwa miongoni mwa nyota watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya mwaka huu kutokana na kuendelea kuonyesha kiwango bora sana hasa baada ya kuifungia Ufaransa mabao mawili muhimu katika michezo miwili ya awali dhidi ya Romania na Albania sasa anakaribia kuvunja rekodi moja kubwa.


    Katika michezo dhidi ya Romania na Albania tayari Payet amefanikiwa kutengeneza jumla ya nafasi 14 za mabao na kuiweka matatani rekodi iliyowekwa mwaka 2004 na nguli wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane. 

    Katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Ureno na Ugiriki kuibuka mabingwa, Zidane alitengeneza nafasi  15 za mabao katika jumla ya michezo mitano kabla ya Ufaransa kutupwa nje ya michuano hiyo na Ugiriki katika hatua ya robo fainali.

    Hii ina maana kwamba sasa Payet anahitaji kutengeneza nafasi mbili zaidi za mabao ili aweze kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kuwahi kutengeneza nafasi nyingi za mabao katika fainali moja za Ulaya (Euro)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PAYET AKARIBIA KUIVUNJA REKODI YA ZIDANE UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top