728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 16, 2016

    WAPYA YANGA SC RUKSA KUKIPIGA SHIRIKISHO

    Dar es Salaam,Tanzania.

    NYOTA wanne wapya wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC,Benno David Kakolanya, Hassan Kessy, Vincent Andrew na Juma Mahadhi sasa wako huru kuichezea klabu hiyo katika michezo ya hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika hii ni baada ya shirikisho la Soka Afrika (CAF),kupitisha majina yao.

    Hii ina maana kwamba Hassan Kessy ataziba mara moja nafasi iliyoachwa wazi na mlinzi Juma Abdul anbaye anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.

    Yanga SC inatarajiwa kuanza kutupa karata yake katika hatua ya makundi kwa kuvaana na Mouloudia Olympique Bejaia, Jumapili Juni 19,katika mchezo wa kundi A utakaochezwa katika uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia,Algeria



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAPYA YANGA SC RUKSA KUKIPIGA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top