728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 16, 2016

    EURO 2016:VARDY,STURRIDGE WAIZIMA WALES

    Lens,Ufaransa.

    ENGLAND imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Kundi B baada ya jioni ya leo kuwafunga ndugu zao wa Wales kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Stade Bollaret jijini Lens.

    Wales ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza baada ya Gareth Bale kufunga kwa mkwaju mkali wa faulo uliokwenda moja kwa moja wavuni licha ya kipa wa England Joe Hart kujaribu kuuzuia.

    Mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na kocha Rod Hodgson ya kuwaingiza Jamie Vardy,Daniel Sturridge na Marcus Rashford yaliipa uhai England na kufanikiwa kupata mabao yake dakika za 56 na 90 kupitia kwa Jamie Vardy na Daniel Sturridge.

    Kwa matokeo hayo England imefanikiwa kuongoza Kundi B baada ya kufikisha pointi nne kufuatia kushuka dimbani mara mbili.Nafasi ya pili inashikwa na Wales yenye pointi tatu sawa na Slovakia,Urusi inaburuza mkia ikiwa na pointi moja.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EURO 2016:VARDY,STURRIDGE WAIZIMA WALES Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top