728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 16, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA ALHAMIS YA LEO JUNI 16,2016

    Alex Song.

    Cavani:Vilabu vya Atletico Madrid na Arsenal vimekwaa kisiki katika mbio zao za kuinasa saini ya mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani baada ya staa huyo wa zamani wa Napoli kusaini mkataba mpya wa miaka minne wa kuendelea kuichezea Paris Saint-Germain.Mkataba huo mpya utamuingizia Cavan,29, mshahara wa £6.25m kwa mwaka na bonasi ya ziada ya £1.25m. (Sky Italia)

    Skrtel:Liverpool imekubali kumuuza kwa kitita cha  £5.5m mlinzi wake, Martin Skrtel,31,kwenda Fenerbahce ya Uturuki. Skrtel,31,ameichezea Liverpool michezo 320 tangu alipojiunga nayo mwaka 2008 akitokea Zenit St Petersburg kwa £6.5m.(Liverpool Echo)

    Nolito:Meneja mpya wa Manchester City Muhispania Pep Guardiola anatamani kumsajili staa wa Celta Vigo, Manuel Agudo Durán maarufu kama Nolito kwa ada ya £14m.Wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya FC Barcelona.(The Sun)

    Mkhitaryan:Kuna kila dalili kuwa Henrikh Mkhitaryan,27, atabaki Borussia Dortmund hii ni baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kuripotiwa kukataa ofa ya £19m toka Manchester United.Msimu huu tayari Borussia Dortmund imeshawapoteza nyota wake wawili Mats Hummels aliyekwenda Bayern Munich na Ilkay Gundogan aliyekwenda Manchester City.(Daily Mirror)

    Balotelli:Mkuu wa kitengo cha masuala ya usajili wa klabu ya Besiktas,Torunogullari Erdal,amesema klabu yake haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Liverpool aliyeishiwa makali Mario Balotelli,24,hii ni baada ya wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola kudai kuwa mteja wake anaweza kwenda Besiktas.(Daily Mail)

    Embolo:Manchester United imeendelea kuonyesha nia ya kumtaka staa wa FC Basel Mswisi Breel Embolo hii ni baada ya miamba hiyo ya Old Trafford kuwa mbioni kutuma ofa ya £19m ili kumsajili.Msimu uliopita Embolo,19, aliifungia FC Basel mabao 13 katila michezo 40 huku pia akifanikiwa kutengeneza mengine tisa.(Manchester Evening News)

    Song:Alex Song huenda akajiunga na Valencia kwa ada ya £7.9m hii ni baada ya Westham United kukataa kumsajili kwa uhamisho wa kudumu.Westham United imechukua uamuzi huo baada ya Song,28, kucheza michezo 12 pekee msimu uliopita wakati akiwa klabuni hapo kwa mkopo kutokana na kuwa majeruhi wa mara kwa Mara.(Fichajes)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA ALHAMIS YA LEO JUNI 16,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top