728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 15, 2016

    UKIYASTAAJABU YA LUIS SUAREZ UTAYAONA YA GONZALO HIGUAIN

    Napoli,Italia.

    Bila shaka kwa sasa duniani Muargentina Gonzalo Higuain na Mruguayi Luis Suarez ndiyo washambuliaji bora zaidi wa katikati.

    Hakuna kipimo kingine cha kuonyesha ubora wao zaidi upachikaji mabao waliouonyesha msimu huu uliomalizika tayari kwa ligi za Italia (Seria A) na Hispania (La Liga) wakiwa na vilabu vyao vya AS Napoli na FC Barcelona.



    HIGUAIN:Higuain,28 ameibuka kinara wa upachikaji mabao baada ya kupachika mabao 36 katika michezo 35 ya Seria A baada ya jana Jumamosi kufunga mabao matatu (hat-trick) na kuiongoza Napoli kuchomoza na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Frosinone.

    Mabao hayo yamemfanya Higuain aweke rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kufunga mabao mengi zaidi katika ligi hiyo ndani ya msimu mmoja akiivunjwa rekodi iliyodumu kwa miaka 66 ya Gunnar Nordahl ya msimu wa 1949-50 ya mabao 35 aliyoiweka akiwa na AC Milan.

    Mabao hayo hayajaenda bure kwani licha ya kumfanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid atwae kiatu cha dhahabu bali pia yameiwezesha AS Napoli kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.


    SUAREZ:Huyu ndiye dunia iko miguuni pake kabisaaaaaaaa,licha ya kuibuka kinara wa mabao La Liga kufuatia kupachika mabao 40 na kuvunja ufalme wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
    Luis Suarez ameongoza pia chati ya upishi wa mabao msimu huu nchini Hispania na kuwa mchezaji wa kwanza kuongoza chati mbili tofauti yaani ya ufungaji ambayo ana mabao 40 na upishi wa mabao ambayo ana assist 16 katika msimu mmoja wa La Liga.

     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UKIYASTAAJABU YA LUIS SUAREZ UTAYAONA YA GONZALO HIGUAIN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top