Leceister,England.
KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya michezo ya NIKE imeendelea kuwapamba nyota wawili wa Leceister City Jamie Vardy na Ryad Mahrez baada ya kuwatengenezea viatu maalumu watakavyovitumia katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea jioni ya leo huko Stamford Blidge.
Viatu hivyo vimepewa jina la VAHREZ,vimebeba ufupisho wa majina ya ubini ya nyota hao waliotoa mchango mkubwa na kuipa Leceister City ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kuusaka kwa miaka 132 bila mafanikio.Kwa pamoja Vardy na Mahrez wamefunga jumla la mabao 41 na kupika mengine 17.
VINAVYOONEKANA!!
Kiatu cha Vardy cha mguu wa kulia ni cheupe wakati cha kushoto ni cheusi,Mahrez kiatu chake cha kulia ni cheusi na cha kushoto ni cheupe..
Pia viatu hivyo vina bendera ya mataifa wanayotokea nyota hao,Viatu vya Vardy vina bendera ya England na vile vya Mahrez vina bendera ya Algeria.
0 comments:
Post a Comment