728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 08, 2016

    MAN CITY YABANWA NA ARSENAL ETIHAD SASA HATI HATI KUIKOSA TOP 4

    Manchester, England.

    Matumaini ya Manchester City kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yametiwa doa baada ya usiku huu kulazimisha sare ya mabao 2-2 na Arsenal nyumbani Etihad.

    Manchester City ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Sergio Aguero kufunga dakika ya 8 akimalizia pasi ya kichwa ya Fernando Luiz Loza "Fernandinho".Dakika mbili baadae Oliver Giroud aliisawazishia Arsenal kwa kichwa akiunganisha kona ya Mohammed Elneny.

    Kipindi cha pili Manchester City ilipata bao la pili kupitia kwa Kevin De Bruyne (51) kabla ya Alexis Sanchez kuisawazishia Arsenal (68).

    Kwa matokeo hayo Arsenal imeendelea kubaki nafasi ya tatu na pointi zake 68,Manchester City ni ya nne ikiwa na pointi 65 huku Manchester United ikiwa nafasi ya tano za pointi zake 63 lakini ina mchezo mmoja mkononi.

    Hii ina maana kwamba ikiwa Manchester United watapata ushindi dhidi ya Westham Jumatano watakuwa wamefikisha pointi 66 na kuitoa Manchester City katika nne bora.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN CITY YABANWA NA ARSENAL ETIHAD SASA HATI HATI KUIKOSA TOP 4 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top