Leceister,England.
Mabingwa wapya wa Ligi Kuu England Leceister City wameendelea
kuonyesha kweli walistahili kitu msimu huu baada ya usiku wa leo wakiwa
nyumbani King Power kuichapa Everton kwa mabao jumla ya 3-1.
Jamie Vardy alianza kuifungia Leceister City dakika ya 5 na kuongeza la pili dakika ya 65 huku Andy
King akipiga la tatu dakika ya 33.Wageni Everton wao wamepata bao lao kupitia
kwa winga wao Kevin Mirallas.
Kwa mabao hayo mawili ya leo Vardy amefikisha mabao 24 na
kuifikia rekodi ya mkongwe Gary Lineker ya kuifungia Leceister City mabao 24
katika msimu mmoja wa Ligi Kuu England.Katika mbio za kuwania tuzo ya mfungaji
bora wa msimu Vardy yuko nafasi ya pili nyuma ya Harry Kane mwenye mabao 25
mpaka sasa.
MATOKEO MENGINE
Sunderland 3-2 Chelsea
Westham 1-4 Swansea City
Crystal Palace 2-1 Stoke City
Aston Villa 0-0 Newcastle
0 comments:
Post a Comment